DE GEA AWASAIDIA MANCHESTER UNITED KUTOKA SARE NA SEVILLA LIGI YA MABINGWA ULAYA UEFA
Mlindalango wa Manchester United David de Gea alifanya kazi ya ziada kuzuia makombora ya wapinzani wao Sevilla Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mechi ya hatua ya 16 bora na kuwasaidia kutoka sare Jumatano. Kipa huyo Mhispania aliwazuia Joaquin Correa na Steven N'Zonzi kufunga kwa ustadi mkubwa, na kisha akatumia mkono mmoja muda mfupi kabla ya mapumziko kuzuia mpira wa kichwa wa Luis Muriel. United, waliokuwa wanacheza mechi yao ya kwanza ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika kipindi cha miaka minne hawakushambulia sana. Romelu Lukaku alipoteza nafasi nzuri zaidi kwao mpira wake ulipopaa juu ya lango mapema, kabla ya nguvu mpya Marcus Rashford kutupa mpira nje dakika za mwisho mwisho. Paul Pogba alianza mechi kwenye benchi, lakini akaingizwa uwanjani dakika 17 kabla ya mechi kumalizika baada ya Ander Herrera kuumia. Sevilla walimaliza mechi wakiwa wameshambulia goli mara 25 lakini mseto wa ustadi wa De Gea na makosa ya washambuliaji wao viliwazuia kuondoka na ushind...