Blatter achunguzwa na FBI kuhusu hongo ya $100m
Kipindi maalumu cha uchunguzi BBC,
Panorama, kimeona ushahidi kwamba rais wa FIFA Sepp Blatter
aliyesimamsishwa kwa muda anachunguzwa na shirika la ujajusi la Marekani
FBI.
Aliyekuwa ameshikia nafasi hiyo kabla ya Blatter, Joao Havelange, alikuwa ni miongoni mwa wanaotuhumiwa kupokea malipo hayo.
Bwana Blatter, amekana kuwa na taarifa yoyote ya sakata hilo, lakini kipindi cha Panorama kimeona barua iliyosainiwa na bwana Joao Havelange ikisema bwana Blatter ana taarifa kamili.
Maoni
Chapisha Maoni