Breaking News: Moto wa Magufuli Watua Tanesco..Wafanyakazi Wasimamishwa Kazi Kutokana na Wizi
Kutoka
shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhusu kuwasimamisha kazi maofisa 7
waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na ubadhirifu.
Akizungumza
leo Dec 6, 2015 mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa
Tanesco, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema…’Ukiacha kero zinazosababisha
na Miundombinu TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadhibisha
wafanyakazi wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja baadhi ya
kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa pamoja na lugha mbaya, wateja
kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma kucheleweshewa huduma, ubadhirifu‘
– Mramba
‘Shirika
linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeanza kuchukua
hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo’ –
Mramba
Kwa
mfano katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi
maofisa 7 waandamizi kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo wizi na
ubadhirifu.Miongoni mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na
kuripotiwa na vyombo vya habari jana.Walioachishwa kazi ni pamoja na
wafanyakazi wa ngazi za Mameneja, wahandisi na wahasibu’ – Mramba
‘Shirika
litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi yeyote atakayebainika
analaghai wateja, anadai rushwa anatoa lugha chafu au huduma mbovu
atawajibishwa mara moja na pale atakapobainika kuachishwa kazi‘Mramba
Maoni
Chapisha Maoni