Mourinho: Itakuwa vigumu kumaliza nne bora
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho
amekiri kwamba itakuwa vigumu kwa timu yake kufuzu kwa Ligi ya Klabu
Bingwa Ulaya msimu ujao baada yao kulazwa 1-0 na Bournemouth nyumbani
Jumamosi.
"Lengo letu ni kumaliza katika nne bora," alisema Mourinho.
"Kabla ya mechi hii, kulikuwa na msingi kufikiria kuwa tulikuwa na uwezo wa kujitoa katika hali hii lakini sasa, labda, itatubidi kufikiria kuhusu sita bora.”
Chelsea kwa sasa wamo alama tatu juu ya eneo la kushushwa daraja, na alama 17 nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.
Mourinho aliongeza: "Nina wasiwasi bila shaka. Lakini hakuna uwezekano kwamba mwishoni mwa msimu Chelsea itakuwa ikipigana kuzuia kushushwa daraja
Maoni
Chapisha Maoni