Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

results half time-full time

Picha
orld Cup - CONCACAF Qualification:: group A March 30 04:06 Honduras ? - ? El Salvador 05:30 Mexico ? - ? Canada World Cup - CONCACAF Qualification:: group B March 30 04:30 Panama ? - ? Haiti 05:00 Costa Rica ? - ? Jamaica World Cup - CONCACAF Qualification:: group C March 30 02:00 Trinidad and Tobago ? - ? Saint Vincent and The Grenadines 02:25 USA ? - ? Guatemala World Cup - AFC Qualification:: group A March 29 74' Palestine 5 - 0 Timor-Leste 31' U.A.E. 0 - 1 Saudi Arabia World Cup - AFC Qualification:: group B March 29 FT Australia 5 - 1 Jordan FT Tajikistan 0 - 1 Kyrgyzstan World Cup - AFC Qualification:: group C March 29 FT China 2 - 0 Qatar 19:00 Maldives ? - ? Bhutan World Cup - AFC Qualification:: group D ...

Brazili kuikabili Paraguay.

Picha
23:30 Colombia ? - ? Ecuador March 30 02:00 Uruguay ? - ? Peru 02:30 Argentina ? - ? Bolivia 02:30 Venezuela ? - ? Chile 03:45 Paraguay ? - ? Brazil    Mechi za kufuzu fainali za kombe la dunia zitakazofanyika mwaka 2018 nchini Urusi, zitachezwa kesho Jumanne Machi 29.   Kwa mujibu wa ratiba Colombia watachuana na Ecuador, Argentina dhidi ya Bolivia, Paraguay watakuwa wakicheza na Brazil , Venezuela watawaalika Chile na Uruguay watakuwa wenyeji wa Peru. Na Michezo ya kirafiki ya kimataifa inatarajia kuendelea tena hii leo, Andorra itachuana na Moldova, Ukraine dhidi ya Wales, Northern Ireland ya kaskanzini na Slovenia,na hapo kesho England watakuwa wenyeji wa Uholanzi. ubeligiji wataialika Ureno, Germany watakuwa wenyeji wa Italy , Ufaransa watakuwa nyumbani dhidi ya Urusi, na Scotland watawakabili Denmark. ya mchezo uliopigwa jana usiku kati ya Romania na Ispania mch...

Ibrahimovic: Klabu za Uingereza zinanitaka

Picha
Mshambuliaji matata wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amesema klabu kadha za Ligi Kuu ya Uingereza zinamtaka. Kwa sasa anachezea mabingwa wa ligi ya Ufaransa Paris St-Germain. Mchezaji huyo wa umri wa miaka 34, ambaye mkataba wake katika klabu hiyo ya Ufaransa utamalizika mwisho wa msimu huu, amehusishwa na kuhamia Manchester United, Chelsea na Arsenal. "Nimekuwa ninatafutwa lakini hebu tusubiri tuone hili litafika wapi,” amesema. “Lakini itahitaji kuwa kama harusi, lazima kila pande zitake sana kuwa pamoja.” Zlatan Ibrahimovic kuihama PSG Ibrahimovic ameshinda ligi katika nchi nne tofauti Ulaya. Alishinda akiwa Uholanzi (Ajax), Italia (Inter Milan, AC Milan), Uhispania (Barcelona) na Ufaransa (PSG).   Baada ya kusaidia PSG kulaza Troyes 9-0 mapema mwezi huu, Ibrahimovic alisema: “Kwa sasa (mambo yalivyo ni kwamba), sitakuwa PSG msimu ujao. Bado nina mwezi mmoja unusu wa kukaa hapa. "Wakibadilisha mnara wa Eiffel na badala yake waweke sa...

Zimbabwe yairarua Swaziland 4 - 0

Picha
Mechi za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya afrika zimepigwa jana kwa michezo kadhaa, Zimbabwe imeirarua Swaziland mabao 4-0 huku Afrika ya kati ikiichapa Madascar goli 2-1. Katika matokeo mengine Equatorial Guinea imechabangwa na mali bao 1-0, na Libya imeizamisha Sao Tome kwa kichapo cha bao 4-0. Michuano hii inaendelea tena leo kwa michezo mbalimbali, miongoni mwa mechi zitakazo pigwa,Malawi itacheza na Guinea, Ethiopia na Algeria, Rwanda itaikabili Maurtius. Katika mechi nyingine Togo itakabana koo na Tunisia wakati Angola watakuwa wenyeji wa D.R Congo, Uganda watawakaribisha Burkina faso, Misri watakuwa wenyeji wa Nigeria, Sudan itachuana na Ivory Coast na Niger itamenyana na Senegal,hizo ni miongon mwa mechi zitakazo pigwa hii leo.  

Mourinho na mikakati kuiboresha Man utd.

Picha
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atachukua nafasi ya Louis van Gaal. Kwa mujibu wa jarida la Don Balonna Mourinho anataka kusajili nyota watatu. Kocha huyo ameshaanza mipango ya usajili kwa kuweka wachezaji kadhaa nyota katika orodha yake akiwemo mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain, kiungo wa Real Madrid James Rodriguez na mshambuliaji wa Juventus Alvaro Morata. Mourinho ameshawahi kufanya kazi na Higuain wakati akiwa Madrid na United wameonyesha kuwa tayari ingawa watalazimika kulipa kitita cha paundi milioni 58 kwa ajili ya kumnasa nyota huyo wa kimataifa wa Argentina. United pia watakabiliwa na upinzani kwa Morata ingawa Madrid wako tayari kumnunua tena kama mkataba unavyotaka ili waje kumuuza kwa kiwango cha juu wakati Rodriguez yeye anatarajiwa kuondoka kiangazi kutokana na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza

Andy Murray atupwa nje -Miami

Picha
Mcheza Tenisi Mwingereza Andy Murray ametupwa nje katika michuano ya wazi ya Miami na Grigor Dimitrov. Murray ametolewa katika raundi ya tatu kwa 6-7, 6-4, 6-3, sawa na alama (1-7 ). Murray mwenye miaka 28, alianza kwa kasi ya juu katika mchezo huo na hadi mapumziko alikuwa akiongoza kwa seti moja. Lakini Mbulgaria Dimitrov mwenye miaka mika 26 alirejea uwanjani na kumdhibiti Murray na kushinda katika mchezo huo. Katika mchezo wa awali, Johanna Konta alikuwa mwanamke Mwingereza wa kwanza Kutinga hatua ya robo fainali katika Miami, huku Heather Watson akipoteza kwa Simona.

Ratiba ya mechi za kufuzu AFCON leo

Picha
Uganda, Rwanda, Burundi na DR Congo ni miongoni timu za mataifa ya Afrika zitakazoshuka dimbani leo kwa mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon. Rwanda watakuwa nyumbani dhidi ya Mauritius nao Uganda wawe nyumbani dhidi ya Burkina Faso. Hii hapa ndiyo ratiba ya mechi za leo. (Kundi L) Malawi 14:30 Guinea Uwanja: Kamuzu Stadium, Blantyre (MWI) (Kundi K) Niger 15:00 Senegal Uwanja: Stade Général S. k., Niamey (NIG) (Kundi A) Togo 15:00 Tunisia Uwanja: KEGUE, Lomé (TOG) (Kundi J) Lesotho 15:00 Seychelles Uwanja: Setsoto Stadium, Maseru (LES) (Kundi H) Rwanda 15:30 Mauritius Uwanja: Kigali, Kigali (RWA) (Kundi A) Liberia 16:00 Djibouti Uwanja: Antonitte Tubman Studium (ATS) , Monrovia (LBR) (Kundi M) Gambia 16:30 Mauritania Uwanja: Bakau, Bakau (GMB) (Kundi B) Angola 17:00 DR Congo Uwanja: 11 de Novembro, Luanda (ANG) (Kundi K) Namibia 17:00 Burundi Uwanja: Sam Nujoma Stadium, Windhoek (NAM) (Kundi J) Et...

Rwanda kushuka dimbani Kigali AFCON

Picha
Timu ya taifa ya Rwanda itashuka dimbani kesho ikilenga kufufua kampeni yake ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Taifa Bingwa Afrika zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon. Rwanda watakuwa wenyeji wa Mauritius kwenye mechi yao ya marudiano Kundi H. Amavubi walilazwa 1-0 na wanavisiwa hao Jumamosi iliyopita na watahitaji sana kushinda kufufua matumaini yao. Mkufunzi wao mkuu Jon McKinstry amesema ana matumaini kwamba wanaweza kufanya mambo dhidi ya Les Dodos. “Kila mtu amesikitishwa na matokeo (ya mechi ya Jumamosi). Lazima tuwe wakweli na kukubali kwamba hatukucheza vyema,” amesema kocha huyo.   Ghana wanaongoza Kundi H baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Msumbiji ugenini Maputo Jumapili, kila timu ikiwa imecheza mechi nne. Mauritius wamo nambari mbili na alama sita, pointi tatu juu ya Rwanda

Mabadiliko katika Instagram yazua hisia kali

Picha
Mabadiliko ya yaliomo katika mtandao wa instagram yamezua hisia kali miongoni mwa watumizi wake. Mtandao huo una mpango wa kuweka ratiba ya mpangilio wa ujumbe hivyobasi kupanga machapisho kulingana na maslahi ya mtumiaji badala ya kuyapanga kulingana na mda. Machapisho mengi ya watu maarufu ambao wana wasiwasi kwamba picha zao huenda zisionekane na watu wengi yamewataka wafuasi wao kufungua kitufe cha ujumbe. Lakini Instagram imesema kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi. ''Tunasikiliza na tunawahakikishia kwamba hakuna mabadiliko yatakayofanyiwa machapisho yenu kwa sasa'',mtandao huo wa usambazaji picha ulisema katika ujumbe wake wa Twitter. Hatua hiyo itauweka sawa mtandao huo na ule wa facebook ambao unamilikiwa na kampuni hiyo. Kwa kufungua kitufe cha ujumbe,wafuasi wa watu hao maarufu watakuwa wakipata ujumbe kila wanapoweka machapisho yao. Watu maarufu kama vile Kylie Jenner na mwanamitindo Cindy Crawford katika siku za hivi karibuni wa...

Video za Justin Bieber zatazamwa mara bilioni 10

Picha
Mwanamuziki Justin Bieber amevunja rekodi ya Vevo kwa video yake kutazamwa mara bilioni 10. Msanii huyo wa Canada ambaye alitoa kibao kipya Purpose in Novemba alipata idadi hiyo katika kipindi cha miaka sita na miezi mitatu au siku 2,316. Kutazamwa kwa video zake mara bilioni 4 kulifanyika baada ya Septemba mwaka jana na mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa katika kilele cha chati ya muziki katika Vevo kwa wiki 19 mfululizo. Justin Bieber,Katy Perry na Taylor Swift ni wasanii pekee wenye video mbili tofauti zilizotazamwa zaidi ya mara bilioni moja kila moja.   Lakini video yake ya What Do You Mean?Itafikisha kutazamwa mara bilioni moja katika kipindi cha wiki chache zijazo,na kumfanya kuwa msanii wa kwanza kuwa na video tatu zilizotazamwa mara bilioni moja. Mnamo mwezi Januari ,David Bowie alivunja rekodi ya Vevo kwa siku moja. Video zake ziliangaliwa mara milioni 51 baada ya kutangazwa kwamba amefariki akiwa na umri wa miak 69.

Wanariadha wala sabuni wakidhania ni chakula

Picha
Wanariadha waliokuwa wanakimbia mbio ndefu za marathon walijipata wamekula sabuni baada ya kudhania kwamba zilikuwa chakula kutokana na kukosa kuelewa lugha ya kiingereza. Takriban wanariadha 20,000 katika mbio za Qinyuan marathon kusini mwa mkoa wa Guangdong nchini Uchina walipata zawadi mda mfupi baada ya kumaliza mbo hizo katika utepe kulingana na gazeti la kila siku nchini humo la Peoples daily. Wakidhania kwamba walikuwa wanakula chakula,wanariadha hao badala yake walikuwa sabuni zilokuwa zikinuka harufu nzuri . Walioshuhudia wanasema kuwa sabuni nyingi zilitupwa kandakando ya barabara huku zikiwa zimeumwa. Tatizo ni kwamba sabuni hizo zilikuwa zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza na hivyobasi wanariadha hao hawakuelewa lugha hiyo kulingana na gazeti hilo. Hatahivyo walioandaa mbio hizo waliomba msamaha.Pakiti za sabuni hizo zilikuwa kama zile za chakula.   Pia kulikuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya majeraha katika mbio hizo huku wanariadha 12,200 wakihita...

Adele aomba msamaha baada ya shabiki kujeruhiwa

Picha
Mwanamuziki wa muziki wa Pop Adele ameomba msamaha baada ya shabiki mmoja kujeruhiwa alipoangukiwa na nyororo katika tamasha la Glasgow. Nyota huyo alikuwa anaendelea na onyesho lake katika ukumbi wa SSE Hydro siku ya ijumaa usiku wakati nyororo hiyo ilipomuangukia mwanamke huyo aliyekuwa amekaa katika eneo la mashabiki. Alichukuliwa na kupelekwa hospitali kama tahadhari kulingana na msemaji wa ukumbi huo. Adele baadaye alituma ujumbe katika mtandao wake wa Tweeter akisema: Pole kwa kusikia kwamba kuna mtu alijeruhiwa katika tamasha yangu usiku. Uchunguzi unaendelea ili kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena.

Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'

Picha
Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha Republicans Donald Trump. Mojawapo ya tukio hilo la kushangaza limefanyika katika kitongoji kimoja cha wakaazi walio na kipato cha chini kiitwacho La Merced. Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.   Wamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico. Desturi hiyo ya kuchoma vikaragosi hutumiwa na wamexico kuelezea hisia zao dhidi ya wanasiasa wenye sera wasizozipenda wakitolea mfano wa jinsi Judas Iscariot, alivyomsaliti Yesu.

Aliyeita mumewe ndovu apewa talaka India

Picha
Mahakama katika mji mkuu wa India imeamua kwamba ni kosa kwa mke kumuita mumewe “ndovu” na kosa hilo linaweza kuwa msingi wa talaka. Mahakama Kuu mjini Delhi imedumisha uamuzi wa mahakama ya chini uliotolewa mwaka 2012 ambao uliidhinisha talaka. Mahakama hiyo ilisema mtu kumuita mumewe ndovu ni “kumtendea ukatili wa kiakili”. Mfanyabiashara aliyeitwa ndovu ana umri wa miaka 35 na alikuwa na uzani wa kilo 100. Alisema mkewe alizoea kumuaibisha kwa kuwa mnene na "kutoweza kutimiza haja yake ya kimapenzi”, vyombo vya habari India vimeripoti. "Hatua ya aliyekata rufaa kumbandika majina na kumrushia matusi mumewe kwa mfano kumuita 'Hathi' [ndovu], 'Mota Hathi' [ndovu mnene], hata kama alikuwa mnene bila shaka ingeathiri hadhi yake na kujiamini kwake,” Jaji Vipin Sanghi alinukuliwa na gazeti la India Today. Mwanamke huyo alikuwa ameambia mahakama hiyo kwamba madai ya mumewe hayakuwa na msingi lakini mahakama haikukubaliana naye.

Amitabh Bachchan ashinda tuzo ya Bollywood

Picha
Nyota wa filamu za Bollywood Amitabh Bachchan na Kangana Ranaut wameshinda mataji makuu katika tuzo za kitaifa za filamu nchini India. Bachchan alishinda tuzo ya muigizaji bora kwa jukumu lake katika Piku huku Ranaut akiwa muigizaji bora upande wa wanawake kwa filamu ya Tanu Weds Manu Returns. Tuzo ya filamu bora lilichukuliwa na Bahubali huku Sanjay Leela Bhansali akijishindia mwelekezaji bora wa filamu ya Bajirao Mastani.   Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na serikali ya India. Hiyo ni tuzo ya nne ya Bachchan.Alijishindia tuzo ya muigizaji bora mwaka 1990,2005 na 2009.

Mtoto wa kwanza katika mji, Italia tangu 1987

Picha
Wenyeji wa mji mmoja mdogo nchini Italia wamekuwa wakisheherekea kuzaliwa kwa mtoto wa kwanza mjini humo tangu miaka ya 1980. Meya wa mji wa Ostana, ulioko Kaskazini mwa Italia ambayo iko katika maeneo ya milima ya Piedmont aliwaongoza wenyeji kusherehekea ndoto yao kukamilika kwa kuzaliwa kwa kizazi kipya. Ostana imeshudia kupungua kwa idadi ya wenyeji wake katika karne iliyopita kwa hivyo kuzaliwa kwa ''Pablo'' katika hospitalini moja ya Turin imeongezea idadi ya wenyeji kufikia 85.   Jarida la La Stampa linasema japo wanasheherekea sio wote wanaoishi mjini humo. Meya Giacomo Lombardo anasema kuwa miaka ya nyuma Ostana ilikuwa na wenyeji 1,000 lakini idadi hiyo ya watu imekuwa ikipungua kila kukicha hadi kufikia 85 sasa. ''Mara ya mwisho mtoto kuzaliwa hapa ni mwisho wa mwaka wa 1987'' Kati ya mwaka wa 1975 -1976 watoto 17 walizaliwa hapa'' Kwa sasa wenyeji wa mji huo wa Ostana wameanza kuweka mikakati ya kuimarish...

Jukwaa laanguka Odinga akihutubu pwani ya Kenya

Picha
Video inayoonesha kiongozi wa upinzani Kenya Bw Raila Odinga na viongozi wengine wakianguka baada ya jukwaa kuporomoka akihutubia mkutano wa hadhara imevuma sana mtandaoni Kenya. Bw Odinga alikuwa akihutubu katika uwanja wa Karisa Maitha mjini Malindi, jimbo la Kilifi katika pwani ya Kenya Alhamisi wiki iliyopita jukwaa lilipodondoka. Mkutano huo ulikuwa wa kuwashukuru wapiga kura kwa kumpigia kura mgombea wa chama chake cha ODM Willy Mtengo kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge uliofanyika Machi 7. Bw Mtengo alishinda uchaguzi huo. Ilikuwa siku moja kabla ya Ijumaa Kuu na Bw Odinga alikuwa akisimulia kuhusu mateso aliyopitia Yesu Kristo. Odinga ampongeza Magufuli, amshauri Lowassa “Wakati huu mimi nilikuwa nimeenda kule Jericho, nikaonyeshwa ile mlima ya majaribio. Pale ambapo shetani alimpeleka Yesu akamuonesha ulimwengu wote. Akamwambia angalia hii yote. Ukikubali kusujudu na kuniabudu hii yote itakuwa ni yako. Lakini Yesu akamwambia wewe nenda mbali shetani .....

Israeli yasalimu amri kuhusu balozi wa Brazil

Picha
Israel imelazimika kufutilia mbali uteuzi wa mlowezi wa kiyahudi kuwa balozi wake nchini Brazil baada ya taifa hilo kukataa kumpokea. Brazil ilipinga na ikakataa katakata kumpokea balozi huyo mteule kutokana na msimamo wake mkali dhidi ya wapalestina. Aidha Brazil ilisema kuwa Dani Dayan ambaye aliongoza unyakuzi wa mashamba ya wapalestina katika ukanda wa ukingo wa Magharibi unamnyima uwezo wa wastani kisiasa. Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, amesma kuwa Dani sasa ataihudumia taifa hilo la kiyahudia katika ubalozi wake wa New York Marekani.   Brazil ilikatalia mbali uteuzi wake mwezi Agosti. Kauli hiyo kali ya Brazil wachanganuzi wanasema kuwa ilielezea wazi msimamo wao dhidi ya unyakuzi wa ardhi ya wapalestina. Awali Netanyahu alikuwa ameonya kuwa angechukua msimamo mkali dhidi ya Brazil iwapo ingeendelea kumkataa balozi huyo.

Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba

Picha
Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya Rais wa Marekani Barack Obama nchini humo. Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa ziara hiyo. Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka kwa Marekani. Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na Marekani mwaka 1961. Kwa Picha: Ziara ya Obama Cuba Obama amtaka Castro asiiogope Marekani Obama na Castro wajibizana Cuba Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”. Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959...

Mshukiwa wa bomu la Brussels aachiwa huru

Picha
Ofisi ya kiongozi wa mashtaka nchini Ubelgiji imemuachilia huru mshukiwa mkuu wa mashambulio ya bomu yaliyotokea juma lililopita jijini Brussels. Kingozi wa mashtaka ya umma anasema hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa mtu anayetambuliwa kama Faycal C ndiye mshukiwa mkuu aliyenaswa na kamera fiche (CCTV) katika eneo lililoathirika. Ofisi hiyo inasema hadi kufikia sasa hizo zilikuwa ni madai tu dhidi ya bwana huyo. Faycal C alikamatwa baada ya mtu kuielezea polisi kuwa alimshuku kuwa ndiye aliyeonekana katika picha fiche CCTV katika uwanja wa ndege wa Zaventem muda mchache kabla ya mlipuko huo uliosababisha maafa makubwa. Kufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji wa kujitolea mhanga akiwa amevalia kofia   Kauli hiyo ya afisi ya kiongozi wa mashtaka imetupilia mbali matumaini ya kumkamata mshukiwa halisi aliyekwepa kutoka eneo la tukio baada ya shambulizi lililoua zaidi ya watu 35. Ibaada ya ...

Milio ya risasi jengo la Bunge Marekani

Picha
Kuna taarifa za milio ya risasi katika viunga vya jengo la Makao Makuu ya Bunge la Congress, US Capitol Hill. Mashuhuda wanasema wameambiwa kwa vipaza sauti kuwa kila mtu ajifiche. Taarifa za hivi punde zinasema mtu huyo mwenye silaha amekamatwa na polisi mmoja amepigwa risasi na kujeruhiwa. Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye eneo jengo la Bunge wameambiwa waendelea kubaki ndani. Ikulu ya White House nayo imefungwa. Msemaji wa Polisi katika Jengo la Bunge hajasema lolote lakini ameahidi polisi kutoa taarifa za tukio hilo wakati wowote.

India kuzindua nambari ya dharura

Picha
i india inatarajiwa kuzindua nambari ya kitaifa ya dharura sawa na 911 nchini Marekani au 999 nchini Uingereza. Nambari hiyo 112,itawaunganisha wapiga kura na maafisa wa polisi ,ambyulensi ,zima moto na huduma nyengine za dharura. Wazo la kuanzisha nambari hiyo limekubaliwa na mamlaka ya mawasiliano kulingana na shirika la habari la India news agency Press Trust of India. Iwapo litaidhinishwa waziri wa mawasiliano ,maafisa wanasema litaanza kufanya kazi katika kipindi cha miezi kadhaa badala ya mwaka. Pendekezo la kuwa na nambari moja ya dharura lilitolewa na kampuni ya kudhibiti mawasiliano nchini India Trai. Kwa sasa India ni lazima ipige nambari kadhaa tofauti. 100 kwa maafisa wa polisi 101 kwa huduma za zima moto 102 kwa huduma za ambyulensi 108 kukabiliana na majanga Idadi ya majimbo kadhaa yameweka nambari nyengine za usaidizi kuwasaidia wanawake,watoto na wazee.Maafisa wanasema kuwa nambari za dharura zitaondolewa polepole wakati nambari hiyo itakapoanza...

Marekani yaifungua iPhone ya Mlipuaji

Picha
Wizara ya Sheria ya Marekani inasema imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone mali ya mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple. Wakili wa Marekani Eileen Decker alisema kuna mtu aliisaidia idara hiyo kuifungua Simu hiyo ya iPhone bila kuathiri data zilizohifadhiwa. Kampuni ya Apple ilikataa kusaidia uchunguzi , kwa kusema ni kuweka ' historia mbaya. Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye, pamoja na mke wake, waliuua watu kumi na wanne kusini mwa California Desemba mwaka jana.

Mkenya aliyejiweka katika picha za wengine

Picha
Mwanamke mmoja kutoka Kenya amejiweka katika msururu wa picha za likizo za watu wengine katika mtandao wake wa facebook Baada ya kushindwa kuwa na uwezo wa kusafiri kwenda barani Asia,Sevelyn Gat alijiweka katika picha karibu na ndege,katika ukuta mkubwa wa Uchina na hekalu moja.   Picha hizo zilizowekwa kwa njia ya nzuri ili zisiweze kubainika kuwa za uongo zilikuwa mbaya zaidi na hivyobasi kuweza kupendwa na mara nyingi sana   Mfanyibiashara wa Nairobi sam Gachuru amejitokeza na kumsaidia kutafuta fedha ili kwenda likizo.   Kulingana na Sich Chirpse Sam aliwasumbua rafikize kuchangisha fedha za mahala pa kulala,nauli bima na pesa za kutumia.   Seve pia amepata kibali chake cha kuzaliwa anemtuma ombi la pasipoti na amepata kufunzwa kama meneja wa mradi.