Jarida la picha za utupu la Playboy 'kuuzwa
Kampuni inayochapisha majarida ya picha za utupu ya Playboy huenda ikauzwa, ripoti nchini Marekani zinasema.
Taarifa hizo zimetokea wiki chache baada ya jarida hilo kutangaza lingeacha kuchapisha picha za utupu likisema ‘haziuzi’.
Mauzo ya majarida hayo yameshuka sana na kufikia 800,000 mwaka jana kutoka 5.6m mwaka 1975.
Ripoti zinasema Investment bank Moelis & Co imeteuliwa kusimamia uuzaji wa biashara ya majarida hayo.
Bw Hugh Hefner alianzisha Playboy mwaka 1953 huku mwigizaji mashuhuri Marilyn Monroe akiwa wa kwanza kupamba ukurasa wa jarida hilo ulioitwa "Playmate of the Month."
Jarida hilo lilipata umaarufu upesi sana.
Taarifa za kifedha za kampuni hiyo huwa hazipatikani kwa urahisi hasa baada ya Bw Hefner na kampuni ya uwekezaji ya Rizvi Traverse Management kufanya kampuni hiyo kuwa ya kibinafsi mwaka 2011.
Lakini wakati wa mabadiliko hayo, Playboy ilikadiriwa kuwa na thamani ya $207m.
Maoni
Chapisha Maoni