Rwanda kushuka dimbani Kigali AFCON
Timu ya taifa ya Rwanda itashuka
dimbani kesho ikilenga kufufua kampeni yake ya kufuzu kwa fainali za
Kombe la Taifa Bingwa Afrika zitakazofanyika mwaka 2017 nchini Gabon.
Amavubi walilazwa 1-0 na wanavisiwa hao Jumamosi iliyopita na watahitaji sana kushinda kufufua matumaini yao.
Mkufunzi wao mkuu Jon McKinstry amesema ana matumaini kwamba wanaweza kufanya mambo dhidi ya Les Dodos.
“Kila mtu amesikitishwa na matokeo (ya mechi ya Jumamosi). Lazima tuwe wakweli na kukubali kwamba hatukucheza vyema,” amesema kocha huyo.
Ghana wanaongoza Kundi H baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Msumbiji ugenini Maputo Jumapili, kila timu ikiwa imecheza mechi nne.
Mauritius wamo nambari mbili na alama sita, pointi tatu juu ya Rwanda
Maoni
Chapisha Maoni