Fidel Castro akosoa ziara ya Obama Cuba

Castro
Aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu wa Cuba Fidel Castro amevunja kimya chake kuhusu ziara ya hivi majuzi ya Rais wa Marekani Barack Obama nchini humo.

Kwenye barua iliyochapishwa katika gazeti la serikali ya nchi hiyo la Granma kiongozi huyo ameonekana kukosoa ziara hiyo.

Fidel, aliyemkabidhi kakake Raul uongozi wa taifa hilo mwongo mmoja uliopita, amesema Cuba haihitaji zawadi zozote kutoka kwa Marekani.
Ziara
Akijibu pendekezo la Bw Obama kwamba wakati umefika wa kuunda urafiki na kuzika kwenye kaburi la sahau masalio ya Vita Baridi bara Amerika, Fidel Castro amewakumbusha wasomaji kuhusu uvamizi wa Bay of Pigs uliofanywa na wakimbizi wa Cuba wakisaidiwa na Marekani mwaka 1961.
Amesema maneno ya Obama ya kuhimiza maridhiano ni sawa na “rojo ya sukari” na kuonya kwamba raia wa Cuba wanaweza kupata “mshtuko wa moyo”.

Fidel Castro, 89, aliongoza Cuba kuanzia 1959 hadi 2008 alipomkabidhi nduguye madaraka.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHELSEA KUWAVAA UNITED BILA YA COSTA

ROGERS NJIA PANDA LIVERPOOL