Mwanamume aliyeteka ndege ya Misri akamatwa
Mwanamume aliyeteka nyara ndege ya shirika la Misri la EgyptAir na kuishurutisha kutua Cyprus amekamatwa, wizara ya mashauri ya kigeni ya Cyprus imetangaza.
Mwanamume huyo alidai kwamba alikuwa na mkanda wa kujilipua na kumwamuru rubani wa ndege hiyo kuielekeza Cyprus au Uturuki.
Ndege hiyo, iliyokuwa safarini kutoka Alexandria hadi mjini Cairo, mwishowe ilitua uwanja wa Larnaca nchini Cyprus.
Abiria karibu wote walikuwa wamefanikiwa kuondoka kutoka kwenye ndege hiyo.
Ripoti zinasema kuwa mtekaji wa ndege ya EgyptAir anataka kuongea na mkewe walietengana naye anayeishi Cyprus ambaye kwa sasa anadaiwa kuelekea katika uwanja huo wa ndege.
EgyptAir: Mtekaji ataka kumuona ''mkewe''
Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades amewaambia waandishi wa habari kwamba tukio hilo la utekaji nyara halikuwa la kigaidi.
Akijibu maswali ya waandishi iwapo mtekaji huyo alishinikizwa na mapenzi, alicheka na kusema, ''kila mara kuna mwanamke anayehusishwa''.
Shirika la habari la Cyprus CYBC linasema kuwa mtekaji huyo huenda alikuwa na malengo yake ya kibinafsi, mtekaji huyo alikuwa na mkewe waliyetengana nchini Cyprus.
Walioshuhudia wanasema kuwa mtekaji huyo alirusha barua katika uwanja huo wa ndege ilioandikwa Kiarabu akiomba ipelekwe kwa mwanamke huyo.
SHIRIKISHO la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kuwarudishia fedha zao kesho Jumanne,
wapenzi wa mpira wa miguu waliokuwa wameshakata tiketi za kushuhudia
mchezo wa kundi G kati ya Tanzania v Chad jijini Dar es salaam. TFF
inawaomba washabiki wa mpira wa miguu waliokua wamekata tiketi za mchezo
huo, kufika kesho Jumanne saa 5 kamili asubuhi katika vituo
walivyonunulia wakiwa na tiketi zao ili waweze kurudishiwa fedha zao.
Zoezi la kuwarudishia fedha washabiki waliokuwa wameshakata tiketi za
mchezo kati ya Tanzania v Chad litafanyika katika vituo vinne vilivyokua
vikiuza tiketi siku ya Jumapili, hivyo wenye tiketi za mchezo huo
wanaombwa kufika na tiketi zao ili waweza kurudishiwa fedha zao. Aidha
TFF inawaomba radhi watanzania na wapenzi wa mpira wa miguu kwa usumbufu
uliojitokeza na kuwataka kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi
hiki ambacho wanasubiria taarifa zaidi kutoka CAF. Chad imejiondoa jana
katika kinyanganyiro cha kuwania kufuzu kwa Fainali za Kombe la Mataifa
Afrika (AFCON) nchini Gabon mwaka 2017, ambapo iliku kundi G na timu za
Misri, Nigeria pamoja na Tanzania.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ
Copy the BEST Traders and Make Money : http://ow.ly/KNICZ
Maoni
Chapisha Maoni