Wa-Mexico wachoma mfano wa 'Trump'
Raia wa Mexico wanaosherehea sikukuu
ya pasaka wamekuwa wakichoma sanamu za mgombea wa kiti cha urais
kupitia chama cha Republicans Donald Trump.
Wakaazi wengi wa La Merced wamejitokeza kushuhudia kuchomwa kwa kikaragosi cha Trump badala ya kile cha yule mfuasi wa Yesu Kristu aliyemsalito Judas Iscariot.
Wamexico wengi hawampendi bw Trump tangu alipotoa matamshi ya kuwakejeli wamexico.
Desturi hiyo ya kuchoma vikaragosi hutumiwa na wamexico kuelezea hisia zao dhidi ya wanasiasa wenye sera wasizozipenda wakitolea mfano wa jinsi Judas Iscariot, alivyomsaliti Yesu.
Maoni
Chapisha Maoni