Marekani yaifungua iPhone ya Mlipuaji
Wizara ya Sheria ya Marekani inasema
imefanikiwa kuzisoma data zilizohifadhiwa kwenye Simu ya iPhone mali ya
mmoja wa walipuaji katika tukio la mauaji la San Bernardino na
kutangaza kuacha mpango wake wa kisheria dhidi ya Kampuni ya Apple.
Kampuni ya Apple ilikataa kusaidia uchunguzi , kwa kusema ni kuweka ' historia mbaya.
Simu hiyo ni mali ya Rizwan Farook ambaye, pamoja na mke wake, waliuua watu kumi na wanne kusini mwa California Desemba mwaka jana.
Maoni
Chapisha Maoni