Mshukiwa wa bomu la Brussels aachiwa huru
Ofisi ya kiongozi wa mashtaka
nchini Ubelgiji imemuachilia huru mshukiwa mkuu wa mashambulio ya bomu
yaliyotokea juma lililopita jijini Brussels.
Ofisi hiyo inasema hadi kufikia sasa hizo zilikuwa ni madai tu dhidi ya bwana huyo.
Faycal C alikamatwa baada ya mtu kuielezea polisi kuwa alimshuku kuwa ndiye aliyeonekana katika picha fiche CCTV katika uwanja wa ndege wa Zaventem muda mchache kabla ya mlipuko huo uliosababisha maafa makubwa.
Kufuatia kauli hiyo polisi wamechapisha upya picha za mshukiwa aliyeonekana akiandamana na washambuliaji wa kujitolea mhanga akiwa amevalia kofia
Kauli hiyo ya afisi ya kiongozi wa mashtaka imetupilia mbali matumaini ya kumkamata mshukiwa halisi aliyekwepa kutoka eneo la tukio baada ya shambulizi lililoua zaidi ya watu 35.
Ibaada ya makumbusho imeratibiwa kufanyika usiku kutwa katika kanisa kuu mjini Brussels.
Maoni
Chapisha Maoni