KUELEKEA MAY 2,MANNY NA MAYWETHER WAONYESHA FAMILIA ZAO
MAYWEATHER NA PACQUIAO WATAMBULISHA 'USINGIZI' WAO USEMI kwamba kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke, ni hivyo hivyo hata mwa mabondia wawili nyota duniani. Zimebaki wiki mbili kabla ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao kukutana ulingoni katika pambano la utajiri mkubwa kwenye historia ya ngumi za kulipwa. Lakini mabondia hao wawili wamehakikisha wanapata muda wa kuwa na watu hao wao wa karibuni zaidi mwishoni mwa wiki. Floyd Mayweather akiwa na mpenzi wake, Doralie Medina (kushoto) na Manny Pacquiao na mkewe Jinkee (kulia) Pacquiao akiwa na mkewe na watoto wa o(kutoka kushoto: Michael, Israel, Emmanuel, Princess na Queen Elizabeth Pacquiao aliungana na mkewe wake wa maisha yote Jinkee na watoto wao watano - Princess, Emmanuel Jnr, Israel, Queen Elizabeth na Michael. Jinkee aliwasili mjini Los Angeles mwezi uliopita, wiki tatu baada ya mumewe kuanza kambi ya maandalizi ya pambano la Mei 2 mjini humo. Wan...