YANGA SC NA ETOILE YAINGIZA MILIONI 231, WENYEWE ‘WARUSHA’ KUTAJA MAPATO RASMI
MCHEZO wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe Shirikisho Afrika, baina
ya wenyeji Yanga SC na Etoile du Sahel ya Tunisia umeingiza Sh. Milioni
231, gift blog imepata hiyo.Hata hivyo, viongozi wa Yanga SC walitupiana mpira jana kuzungumzia mapato ya mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 1-1 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilano ya Yanga SC, Jerry Muro alisema apigiwe Mhasibu azungumzie mapato.
Hata hivyo, Mhasibu wa Yanga SC naye akampasia mpira Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto
Kutwa nzima ya leo (jana) nimekuwa nikiwafuatilia Yanga SC wanipe taarifa ya mapato ya mechi yao niitoe kwenye vyombo vya Habari, bahati mbaya sikuwapata,”alisema Baraka.
Hata hivyo, taarifa za ndani ambazo gift blog imezipata ni kwamba mechi hiyo imeingiza Sh. Milioni 231, ingawa mchanganuo haukupatikana.
Maoni
Chapisha Maoni