Umoja wa Mataifa unasema unahofia
kuwa huenda watu 800 walifariki siku ya Jumapili, pale mashua waliyokuwa
wakilitumia kuvuka bahari ya Mediterenean ilipozama karibu na Libya.
Shirika
la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR, limekuwa
likizungumza na manusura baada ya kuwasili katika kisiwa cha Sicily
mapema leo Jumanne. Mkuu wa sera kwenye Muungano wa
Ulaya Federica Mogherini anasema kuwa pana haja ya kuwepo hatua za
haraka ili kushughulikia suala kuhusu wahamiaji katika bahari ya
Mediterranean, huku akizindua mikakati kumi ya mpango wa kutanzua vifo
vya wahamiaji.
Mogherini, anasema kuwa mipango hiyo ni hatua kubwa
ya kuzuia kupotea kwa maisha ya watu. Majukumu ya muungano huo ni
kuzidisha operesheni ya uokozi, pamoja na mipango mipya ya kuharibu
mashua zinazotumiwa na walanguzi wa binadamu wanaowavusha watu baharini.
NGASA AKIFANYA YAKE JANA TAIFA MMHH JAVUUUUUUUUUUUUUU MSUVAA HUYOOOOOOOOOOOOO TELELAA AKIWA KAZINI HAMISI TAMBWE AKIMKIMBIZA MTU JANA IVAN RAKITIC AKISHANGILIA KUWAUWA MAN CITY JANA
Chelsea wanatumai kwamba mshambuliaji Loic Remy atacheza katika mechi dhidi ya manchester United baada ya kukosa mechi dhidi ya QPR na jeraha la mguu. Mshambuliaji hatari wa timu ya soka ya chelsea didier Drogbaaaa akishangilia moja ya mabao yake Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa hatocheza lakini anaweza kurudi dhidi ya Arsenal wiki ijayo. Mkufunzi wa kilabu ya manchester United Luois Van Gaal atawakosa wachezaji wake wanne akiwemo Michael carrick,Daley Blind,Phil Jones na Marcos Rojo. Jonny Evans na Chris Smalling wanahudumia marufuku huku Paddy McNair na Tyler Blackett ni wachezaji wa pekee wa safu ya ulinzi wa kiungo cha kati waliosalia.
Kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers yupo kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kutwaa taji lolote katika misimu mitatu ya mwanzo ya kuwanoa vijogoo hao wa Anfield. Hii ni rekodi ambayo haijawahi tokea kwa kocha yeyote tangu mwaka 1950 ndani ya kikosi hicho. ,Je ni wachezaji wasiokidhi viwango?,au ni mbinu za kocha zilizogota mwisho?hayo ni baadhi ya maswali ambayo bado hayana majibu,huku Brendan Rodgers hata kama anakula basi chakula hakishuki uzuri kwani hajui nini hatima yake kufuatia kuboronga huko.
Maoni
Chapisha Maoni