KUELEKEA MAY 2,MANNY NA MAYWETHER WAONYESHA FAMILIA ZAO
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
MAYWEATHER NA PACQUIAO WATAMBULISHA 'USINGIZI' WAO
USEMI kwamba kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma yake kuna mwanamke, ni hivyo hivyo hata mwa mabondia wawili nyota duniani.
Zimebaki
wiki mbili kabla ya Floyd Mayweather na Manny Pacquiao kukutana
ulingoni katika pambano la utajiri mkubwa kwenye historia ya ngumi za
kulipwa.
Lakini mabondia hao wawili wamehakikisha wanapata muda wa kuwa na watu hao wao wa karibuni zaidi mwishoni mwa wiki.
Floyd Mayweather akiwa na mpenzi wake, Doralie Medina (kushoto) na Manny Pacquiao na mkewe Jinkee (kulia)
Pacquiao akiwa na mkewe na watoto wa o(kutoka kushoto: Michael, Israel, Emmanuel, Princess na Queen Elizabeth
Pacquiao
aliungana na mkewe wake wa maisha yote Jinkee na watoto wao watano
- Princess, Emmanuel Jnr, Israel, Queen Elizabeth na Michael.
Jinkee
aliwasili mjini Los Angeles mwezi uliopita, wiki tatu baada ya mumewe
kuanza kambi ya maandalizi ya pambano la Mei 2 mjini humo. Wanandoa hao,
hivi karibuni walinunua jumba eneo la Beverly Hills kwa Pauni Milioni
8.4.
Ndoa yao ikiwa ina umri wa miaka 15 sasa, wapendanao hao ndiyo mastaa maarufu zaidi nchini Ufilipino
Mayweather akiwa amepozi na vazi lake maarufu la TMT alipokuwa mapumzikoni mwishoni mwa wiki
Anafahamika kama 'Bad Medina' kwenye wasifu wa akaunti zake za mitandao ya kijamii, huyo ndiye mpenzi wa Mayweather .
Mabindia wote walitarajiwa leo kuanza wiki ya mwisho ya mazoezi magumu kuelekea pambano lao.
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Maoni
Chapisha Maoni